Alhamisi ya 19 ya Mwaka
· Mwaka C · Juma la 3 la Zaburi
Somo la Kwanza
Eze 12:1–12Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 78:56–59, 61–62Usiyasahau matendo ya Mungu.
Walimjaribu Mungu Aliye juu wakamwasi.
Wala hawakuzishika shuhuda zake.
Bali walirudi nyuma, wakahaini kama baba zao;
Wakaepea kama upinde usiofaa.
K. Usiyasahau matendo ya Mungu.
Wakamkasirisha kwa mahali pao pa juu,
Wakamtia wivu kwa sanamu zao,
Mungu akasikia, akaghadhibika,
Akamkataa Israeli kabisa.
K. Usiyasahau matendo ya Mungu.
Akaziacha nguvu zake kutekwa,
Na fahari yake mkononi mwa mtesi.
Akawatoa watu wake wapigwe kwa upanga;
Akaughadhibikia urithi wake.
K. Usiyasahau matendo ya Mungu.
Shangilio la Injili
Kol 3:16, 17Neno la Kristu likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote; mkimshukuru Mungu Baba kwa Yeye.
Aleluya.
Injili
Mt 18:21–19:1Mtumwa yule akatoka, akamwona mmoja wa waojli wake akaanguka miguuni pake, akamsihi, akisema, Nivumilie, nami nitakulipa yote pia. Lakini hakutaka, akaenda, akamtupa kifungoni, hata atakapoilipa ile deni. Basi wajoli wake walipoyaona yaliyotendeka, walisikitika sana, wakaenda wakamweleza bwana wao yote yaliyotendeka. Ndipo bwana wake akamwita akamwambia, Ewe mtumwa mwovu, nalikusamehe wewe deni ile yote, uliponisihi; nawe, je! Haikukupasa kumrehemu mjoli wako, kama mimi nilivyokurehemu wewe? Bwana wake akaghadhibika, akampeleka kwa watesaji, hata atakapoilipa deni ile yote. Ndivyo na Baba yangu wa mbinguni atakavyowatenda ninyi, msiposamehe kwa mioyo yenu kila mtu ndugu yake. Ikawa Yesu alipomaliza maneno hayo, akatoka Galilaya akafika mipaka ya Uyahudi, ng’ambo ya Yordani.
Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni