Sherehe ya Moyo Mtakatifu wa Yesu Kristo
· Mwaka C
Somo la Kwanza
Eze 34:11-16Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 23Bwana ndiye mchungaji wangu sitapungukiwa na kitu.
Bwana ndiye mchungaji wangu,
Sitapungukiwa na kitu;
Katika malisho ya majani mabichi hunilaza,
Kando ya maji ya utulivu huniongoza.
K. Bwana ndiye mchungaji wangu sitapungukiwa na kitu.
Hunihuisha nafsi yangu; na kuniongoza
Katika njia za haki kwa ajili ya jina lake.
Naam, nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti,
Sitaogopa mabaya;
Kwa maana Wewe upo pamoja nami,
Gongo lako na fimbo yako vyanifariji.
K. Bwana ndiye mchungaji wangu sitapungukiwa na kitu.
Waandaa meza mbele yangu,
Machoni pa watesi wangu.
Umenipaka mafuta kichwani pangu,
Na kikombe changu kinafurika.
K. Bwana ndiye mchungaji wangu sitapungukiwa na kitu.
Hakika wema na fadhili zitanifuata
Siku zote za maisha yangu;
Nami nitakaa nyumbani mwa Bwana milele.
K. Bwana ndiye mchungaji wangu sitapungukiwa na kitu.
Somo la Pili
Rum 5:5-11Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Shangilio la Injili
Yn 10: 14Mimi ndimi mchungaji mwema;asema Bwana; nao walio wangu nawajua; nao walio wangu wanijua mimi;
Aleluya.
Injili
Lk 15: 3-7Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni