Jumatano ya 12 ya Mwaka
· Mwaka C · Juma la 4 la Zaburi
Somo la Kwanza
2 Fal 22:8–13, 23:1–3Ikawa, mfalme alipokwisha kuyasikia maneno ya kitabu hicho cha torati, alirarua nguo zake. Mfalme akamwamuru Hilkia kuhani, na Ahikamu, mwana wa Shafani mwandishi, na Asaya, mtumishi wa mfalme, akasema, Enendeni, mkamwulize Bwana kwa ajili ya Yuda yote, katika habari za maneno ya kitabu hiki kilichoonekana; kwa kuwa hasira ya Bwana ni kubwa aliyotukasirikia, kwa sababu baba zetu hawakuyaangalia maneno ya kitabu hiki, kufanya kama hayo yote tuliyoandikiwa.
Kisha, mfalme akatuma wajumbe, nao wakamkusanyia wazee wote wa Yuda na wa Yerusalemu. Mfalme akapanda kwenda nyumbani kwa Bwana, na watu wote wa Yuda, nao wote waliokaa Yerusalmeu. Mfalme akapanda kwenda nyumbani kwa Bwana, na watu wote wa Yuda, nao wote waliokaa Yerusalemu, pamoja naye, na makuhani, na manabii, na watu wote, wadogo kwa wakubwa; akasoma masikioni mwao maneno yote ya kitabu cha agano kilichoonekana katika nyumba ya Bwana. Mfalme akasimama karibu na nguzo, akafanya agano mbele za Bwana, kumfuata Bwana, na kuyashika maagizo yake, na shuhuda zake, na amri zake, kwa moyo wake wote, na kwa roho yake yote, na kuyathibitisha maneno ya agano hilo yaliyoandikwa katika kitabu hicho; nao watu wote wakalikubali agano lile.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 119:33–37, 40Ee Bwana, unifundishe njia ya amri zako.
Ee Bwana, unifundishe njia ya amri zako,
Nami nitaishika hata mwisho.
Unifahamishe nami nitaishika sheria yako,
Naam, nitaitii kwa moyo wangu wote.
K. Ee Bwana, unifundishe njia ya amri zako.
Uniendeshe katika mapito ya maagizo yako,
Kwa maana nimependezwa nayo.
Unielekeze moyo wangu na shuhuda zako,
Wala usiielekee tamaa.
K. Ee Bwana, unifundishe njia ya amri zako.
Unigeuze macho yangu nisitazame visivyofaa,
Unihuishe katika njia yako.
Tazama, nimeyatamani mausia yako,
Unihuishe kwa haki yako.
K. Ee Bwana, unifundishe njia ya amri zako.
Shangilio la Injili
Yn 17:17Neno lako kweli, ee Bwana, ututakase kwa ile kweli.
Aleluya.
Injili
Mt 7:15–20Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni