Ijumaa ya 10 ya Mwaka
· Mwaka C · Juma la 2 la Zaburi
Somo la Kwanza
1Fal 19:9, 11-16Na tazama, sauti ikamjia, kusema, Unafanya nini hapoa, Eliya? Akasema, Nimeona wivu mwingi kwa ajioi ya Bwana, Mungu wa majeshi; kwa kuwa wana wa Israeli wameyaacha maagizo yako, na kuzivunja madhabahu zako, na kuwaua manabii wako kwa upanga; name nimesalia, mimi peke yangu; nao wanitafuta roho yangu waiondoe.
Bwana akamwambia, Enenda, urudi njia ya njwangwa la Dameski; ukifika, mtie mafuta Hazaeli awe mfalme wa Shamu. Na Yehu mwana wa NImshi mtie mafuta awe mfalme wa Israeli; na Elisha mwana wa Shafati wa Abel-Mehola mtie mafuta awe nabii mahali pako.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 27:7-9, 13-14Usinifiche uso wako, Ee Bwana.
Ee Bwana, usikie, kwa sauti yangu ninalia,
Unifadhili, unijibu.
Uliposema, Nitafuteni uso wangu,
K. Usinifiche uso wako, Ee Bwana.
Usinifiche uso wako,
Usijiepushe na mtumishi wako kwa hasira.
Umekuwa msaada wangu, usinitupe,
Wala usiniache, ee Mungu wa wokovu wangu.
K. Usinifiche uso wako, Ee Bwana.
Naamini ya kuwa nitauona wema wa Bwana,
Katika nchi ya walio hai.
Umngoje Bwana, uwe hodari,
Upige moyo konde, naam, umngoje Bwana.
K. Usinifiche uso wako, Ee Bwana.
Shangilio la Injili
Ebr 4:2Neno la Mungu li hai tena li na nguvu, li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo.
Aleluya.
Injili
Mt 5:27-32Imenenwa pia, Mtu akimwacha mkewe, na ampe hati ya talaka; lakini mimi nawaambia, Kila mtu amwachaye mkewe, isipokuwa kwa habari ya uasherati, amfanya kuwa mzinzi; na mtu akimwoa yule aliyeachwa, azini.
Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni