· Mwaka C
Somo la Kwanza
1Kor. 11:17 – 26, 33Kwa maana mimi nalipokea kwa Bwana niliyowapa nanyi, ya kuwa Bwana Yesu usiku ule aliotolewa alitolewa alitwaa mkate, naye akiisha kushukuru akaumega, akasema, huu ndio mwili wangu ulio kwa ajili yenu; fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu. Na vivi hivi baada ya kula akakitwaa kikombe, akisema, kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu; fanyeni hivi kila mnywapo, kwa ukumbusho wangu. Maana kila mwulapo mkate huu na kukinywa kikombe hiki, mwaitangaza mauti ya Bwana hata ajapo. Kwa hiyo, ndugu zangu, mkutanikapo mpate kula, mngojane.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab. 40:6 – 8, 16Mwaitangaza mauti ya Bwana hata ajapo.
Dhabihu na matoleo hukupendezwa nazo,
Masikio yangu umeyazibua,
Kafara na sadaka za dhambi hukuzitaka.
Ndipo niliposema, Tazama nimekuja.
K. Mwaitangaza mauti ya Bwana hata ajapo.
Katika gombo la chuo nimeandikwa,
Kuyafanya mapenzi yako,
Ee Mungu wangu, ndiyo furaha yangu
Naam, sheria yako imo moyoni mwangu.
K. Mwaitangaza mauti ya Bwana hata ajapo.
Nimehubiri habari za haki katika kusanyiko kubwa,
Sikuizuia midomo yangu; Ee Bwana, unajua.
K. Mwaitangaza mauti ya Bwana hata ajapo.
Washangilie, wakafurahie,
Wote wakutafutao.
Waupendao wokovu wako
Waseme daima. Atukuzwe Bwana.
K. Mwaitangaza mauti ya Bwana hata ajapo.
Shangilio la Injili
Yn. 14:5Bwana anasema: mimi ndimi njia, na ukweli na uzima; mtu haji kwa Baba ila kwa njia ya Mimi.
Aleluya.
Injili
Lk. 7:1 – 10Hata alipokuwa si mbali na nyumba yake, yule akida alituma rafiki kwake, akamwambia, Bwana, usijisumbue, maana mimi sistahili wewe uingie chini ya dari yangu; kwa hiyo nilijiona sistahili mwenyewe kuja kwako; lakini, sema neno tu, na mtumwa wangu atapona. Kwa maana mimi nami ni mtu niliyewekwa chini ya mamlaka, mwenye askari chini yangu; nikimwambia huyu, Nenda, huenda; na huyu, Njoo, huja; na mtumwa wangu, Fanya hivi, kufanya. Yesu aliposikia hayo alimstaajabia, akaugeukia mkutano uliokuwa ukimfuata, akasema, Nawaambia, hata katika Israeli sijaona Imani kubwa namna hii. Na wale waliotumwa waliporudi nyumbani, wakamkuta yule mtumwa ni mzima.
Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni