Jumatatu ya Pasaka
· Mwaka C
Somo la Kwanza
Mdo 2:14, 22–32Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 16:1–2, 5, 7–11Mungu unihifadhi mimi, kwa maana nakukimbilia wewe.
Mungu unihifadhi mimi,
Kwa maana nakukimbilia Wewe.
Nimemwambia Bwana, Ndiwe Bwana wangu;
Bwana ndiye fungu la posho langu, na la kikombe changu;
Wewe unaishika kura yangu.
K. Mungu unihifadhi mimi, kwa maana nakukimbilia wewe.
Nitamhimidi Bwana aliyenipa shauri,
Naam, mtima wangu umenifundisha usiku.
Nimemweka Bwana mbele yangu daima,
Kwa kuwa yako kuumeni kwangu, sitaondoshwa.
K. Mungu unihifadhi mimi, kwa maana nakukimbilia wewe.
Kwa hiyo moyo wangu unafurahi,
Nao utukufu wangu unashangilia,
Naam, mwili wangu nao utakaa kwa kutumaini.
Maana hutaiachaia kuzimu nafsi yangu.
Wala hutamtoa mtakatifu wako aone uharibifu.
K. Mungu unihifadhi mimi, kwa maana nakukimbilia wewe.
Utanijulisha njia ya uzima;
Mbele za uso wako ziko furaha tele;
Na katika mkono wako wa kuume mna mema ya milele.
K. Mungu unihifadhi mimi, kwa maana nakukimbilia wewe.
Shangilio la Injili
Zab 118:24Siku hii ndiyo aliyoifanya Bwana, tutaishangilia na kuifurahia.
Aleluya.
Injili
Mt 28:8–15Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni