Alhamisi baada ya Epifania
· Mwaka C · Juma la 2 la Zaburi
Somo la Kwanza
1Yoh 4:19-5:4Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 72:1-2, 14-15Mataifa yote ya dunia watakusujudia, Ee Bwana.
Ee Mungu, mpe mfalme hukumu yako,
Na mwana wa mfalme haki yako.
Atawaamua watu wako kwa haki,
Na watu wako walioonewa kwa hukumu.
K. Mataifa yote ya dunia watakusujudia, Ee Bwana.
Atawakomboa nafsi zao na kuonewa na udahlimu,
Na damu yao ina thamani machoni pake.
Na wamwombee daima;
Na kumbariki mchana kutwa.
K. Mataifa yote ya dunia watakusujudia, Ee Bwana.
Jina lake na lidumu milele,
Pindi ling’aapo jua jina lake liwe na wazao;
Mataifa yote na wajibariki katika yeye,
Na kumwita heri.
K. Mataifa yote ya dunia watakusujudia, Ee Bwana.
Shangilio la Injili
Lk 7:16Nabii mkuu ametokea kwetu; na Mungu amewaangalia watu wake.
Aleluya.
Injili
Lk 4:14-22Akaenda Nazareti, hapo alipolelewa; na siku ya sabato akaingia katika sinagogi kama ilivyokuwa desturi yake, akasimama ilia some. Akapewa chuo cha nabii Isaya, akakifungua chuo, akatafuta mahali palipoandikwa, Roho wa Bwana yu juu yangu, kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, na vipofu kupata kuona tena, kuwaacha huru waliosetwa, na kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa. Akakifunga chuo, akamrudishia mtumishi, akaketi; na watu wote waliokuwamo katika sinagogi wakamkazia macho. Akaanza kuwaambia, Leo maandiko haya yametimia masikioni mwenu. Wakamshuhudia wote, wakiyastaajabia maneno ya neema yaliyotoka kinywani mwake.
Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni