Dominika ya 3 ya Majilio
· Mwaka C · Juma la 3 la Zaburi
Somo la Kwanza
Sef 3:14-18Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Isa 12:2-6Paza sauti, piga kelele maana mtakatifu wa Israeli ni mkuu kati yako.
Tazama, Mungu ndiye wokovu wangu;
Nitatumaini wala sitaogopa;
Maana Bwana ni nguvu zangu na wimbo wangu.
Naye amekuwa wokovu wangu.
Basi, kwa furaha mtateka maji
Katika visima vya wokovu.
K. Paza sauti, piga kelele maana mtakatifu wa Israeli ni mkuu kati yako.
Mshukuruni Bwana, liitieni jina lake;
Yatangazeni matendo yake kati ya mataifa
Litajeni jina lake kuwa limetukuka.
K. Paza sauti, piga kelele maana mtakatifu wa Israeli ni mkuu kati yako.
Mwimbieni Bwana, kwa kuwa ametenda makuu;
Na yajulikane haya katika dunia yote.
Paza sauti, piga kelele, mwenyeji wa Sayuni;
Maana Mtakatifu wa Israeli ni mkuu kati yako.
K. Paza sauti, piga kelele maana mtakatifu wa Israeli ni mkuu kati yako.
Somo la Pili
Flp 4:4-7Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Shangilio la Injili
Lk 4:18Roho wa Bwana yu juu yangu, amenituma kuwahubiri maskini habari njema.
Aleluya.
Injili
Lk 3:10-18Basi, watu walipokuwa wakingoja yatakayotokea, wote wakiwaza-waza mioyoni mwao habari za Yohana, kama labda yeye ndiye Kristo, Yohane alijibu akawaambia wote, Kweli mimi nawabatiza kwa maji; lakini anakuja mtu mwenye nguvu kuliko mimi, ambaye mimi sistahili kuulegeza ukanda wa viatu vyake; yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto; ambaye pepeo lake li mkononi mwake, naye atausafisha sana uwanda wake, na kuikusanya ngano ghalani mwake, bali makapi atayateketeza kwa moto usiozimika. Basi, kwa maonyo mengine mengi aliwahubiri watu.
Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni