Jumanne ya 2 ya Majilio
· Mwaka C · Juma la 2 la Zaburi
Somo la Kwanza
Isa 40:1–11Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 96:1–3, 10–13Tazameni, Bwana Mungu atakuja kama shujaa.
Mwimbieni Bwana wimbo mpya,
Mwimbieni Bwana, nchi yote.
Mwimbieni Bwana likarikini jina lake,
Tangazeni wokovu wake siku kwa siku.
K. Tazameni, Bwana Mungu atakuja kama shujaa.
Wahubirini mataifa habari za utukufu wake,
Na watu wote habari za maajabu yake.
Semeni katika mataifa, Bwana ametamalaki,
Atawahukumu watu kwa adili.
K. Tazameni, Bwana Mungu atakuja kama shujaa.
Mbingu na zifurahi, nchi na ishangilie,
Bahari na ivume na vyote viijazavyo.
Mashamba na yashangilie, na vyote vilivyomo,
Ndipo miti yote ya mwituni iimbe kwa furaha.
K. Tazameni, Bwana Mungu atakuja kama shujaa.
Mbele za Bwana, kwa maana anakuja,
Kwa maana anakuja aihukumu nchi,
Atahukumu ulimwengu kwa haki,
Na mataifa kwa uaminifu wake.
K. Tazameni, Bwana Mungu atakuja kama shujaa.
Shangilio la Injili
ShangilioSiku ya Bwana i karibu, Tazama atakuja kutuokoa.
Aleluya.
Injili
Mt 18:12–14Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni