Sikukuu ya Kutabarukiwa Basilika la Laterani
· Mwaka B
Somo la Kwanza
Eze 43:1-2, 4-7Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 122:1-5, 7-8Nalifurahi waliponiambia,
Na twende nyumbani kwa Bwana.
Miguu yetu imesimama Ndani ya malango yako, Ee Yerusalemu.
(K)Nalifurahi waliponiambia,na twende nyumbani kwa Bwana.
Ee Yerusalemu uliyejengwa Kama mji ulioshikamana,
Huko ndiko walikopanda kabila, Kabila za Bwana;
Ushuhuda kwa Israeli, Walishukuru jina la Bwana.
(K)Nalifurahi waliponiambia,na twende nyumbani kwa Bwana.
Maana huko viliwekwa viti vya hukumu, Viti vya enzi vya mbari ya Daudi.
Amani na ikae ndani ya kuta zako, Na kufanikiwa ndani ya majumba yako.
Kwa ajili ya ndugu zangu na rafiki zangu Niseme sasa, Amani ikae nawe.
(K)Nalifurahi waliponiambia,na twende nyumbani kwa Bwana.
Somo la Pili
1Kor 3:9-11, 16-17Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu, nay a kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu? Kama mtu akiliharibu hekalu la Mungu, Mungu atamharibu mtu huyo. Kwa maana hekalu la Mungu ni takatifu, ambalo ndilo ninyi.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Shangilio la Injili
2Nya 7:16Nimeichagua nyumba hii na kuitakasa, asema Bwana, ili kwamba jina langu lipate kuwako huko milele.
Aleluya.
Injili
Yn 2:13-22Basi Wayahudi wakajibu, wakamwambia, Ni ishara gani utuonyeshayo, kwamba unafanya haya? Yesu akajibu, akawaambia, Livunjeni hekalu hili, name katika siku t atu nitalisimamisha. Basi Wayahudi wakasema, Hekalu hili lilijengwa katika muda wa miaka arobaini na sita, nawe utalisimamisha katika siku tatu? Lakini yeye alinena habari za hekalu la mwili wake. Basi alipofufuka katika wafu, wanafunzi wake wakakumbuka ya kuwa alisema hivi, wakaliamini lile andiko na lile neno alilolinena Yesu.
Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (1)
Betram Mushi · 9 Novemba 2021
Milele....Amina...Tumshukuru..Mungu.