Ijumaa ya 30 ya Mwaka
· Mwaka B · Juma la 2 la Zaburi
Somo la Kwanza
Rum 9:1-5Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 147:12-15, 19-20Msifu Bwana, Ee Yerusalemu.
Msifu Bwana, Ee Yerusalemu;
Msifu Mungu wako, Ee Sayuni.
Maana ameyakaza mapingo ya malango yako,
Amewabariki wanao ndani yako.
K. Msifu Bwana, Ee Yerusalemu.
Ndiye afanyaye Amani mipakani mwako,
Akushibishaye kwa unono wa ngano.
Huipeleka amri yake juu ya nchi,
Neno lake lapiga mbio sana.
K. Msifu Bwana, Ee Yerusalemu.
Humhubiri Yakobo neno lake,
Na Israeli amri zake na hukumu zake.
Hakulitendea taifa lolote mambo kama hayo,
Wala hukumu zake hawakuzijua.
Aleluya.
K. Msifu Bwana, Ee Yerusalemu.
Shangilio la Injili
Zab 119:34Unifahamishe nami nitaishika sheria yako, nitaitii kwa moyo wangu wote.
Aleluya.
Injili
Lk 14:1-6Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (1)
Betram Mushi · 29 Oktoba 2021
Milele....Amina...tumshukuru..Mungu.