Jumanne ya 20 ya Mwaka
· Mwaka C
Somo la Kwanza
Eze 28:1-10Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Kumb 32:26-28,30,35-36Naua Mimi, nahuisha Mimi.
Nalisema, Ningewatawanyia mbali, Ningekomesha kumbukumbu lao kati ya wanadamu;
Isipokuwa naliogopa makamio ya adui, Adui zao wasije wakafikiri uongo,
K. Naua Mimi, nahuisha Mimi.
Wasije wakasema, Mkono wetu umetukuka, Wala Bwana hakuyafanya haya yote.
Maana hawa ni taifa wasio shauri, Wala fahamu hamna ndani yao.
K. Naua Mimi, nahuisha Mimi.
Mmoja angefukuzaje watu elfu, Wawili wangekimbizaje elfu kumi,
Kama Mwamba wao asingaliwauza, Kama Bwana asingaliwatoa?
K. Naua Mimi, nahuisha Mimi.
Maana siku ya msiba wao imekaribia, Na mambo yatakayowapata yatafanya haraka.
Kwa kuwa Bwana atawaamua watu wake, Atawahurumia watumwa wake,
K. Naua Mimi, nahuisha Mimi.
Shangilio la Injili
2Kor 8:9Bwana wetu Yesu Kristo alivyokuwa maskini kwa ajili yenu, ingawa alikuwa tajiri, ili kwamba ninyi mpate kuwa matajiri kwa umaskini wake.
Aleluya
Injili
Mt 19:23-30Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni