Alhamisi ya 22 ya Mwaka
· Mwaka B · Juma la 2 la Zaburi
Somo la Kwanza
Kol 1:9-14Naye alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo lake; ambaye katika yeye tuna ukombozi, yaani, msamaha wa dhambi.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 98:2-6Bwana ameufunua wokovu wake.
Bwana ameufunua wokovu wake,
Machoni pa mataifa ameidhihirisha haki yake.
Amezikumbuka rehema zake,
Na uaminifu wake kwa nyumba ya Israeli.
K. Bwana ameufunua wokovu wake.
Miisho yote ya dunia imeuona
Wokovu wa Mungu wetu.
Mshangilieni Bwana, nchi yote,
Inueni sauti, imbeni kwa furaha, imbeni zaburi.
K. Bwana ameufunua wokovu wake.
Mwimbieni Bwana zaburi kwa kinubi,
Kwa kinubi na sauti ya zaburi.
Kwa panda na sauti ya baragumu.
Shangilieni mbele za mfalme, Bwana.
K. Bwana ameufunua wokovu wake.
Shangilio la Injili
1 Pet 1:25Neno la Bwana hudumu hata milele, na neno hilo ni neno lile jema lililohubiriwa kwenu.
Aleluya.
Injili
Lk 5:1 – 11Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (1)
Hosea Kimutai · 2 Septemba 2021
Masomo ya tarehe 5