Ijumaa ya 16 ya Mwaka
· Mwaka B · Juma la 4 la Zaburi
Somo la Kwanza
Kut 20: 1-17Usilitaje bure jina la Bwanu, mungu wako, maana Bwana hatamhesabia kuwa hana hatia mtu alitajaye jina lake bure. Ikumbuke siku ya sabato uitakase. Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote; lakini siku ya saba ni sabato ya Bwana, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yo yote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako. Maana, kwa siku sita Bwana alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba; kwa hiyo Bwana akaibarikia siku ya sabato akaitakasa.
Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na Bwana. Mungu wako. Usiue. Usizini. Usiibe. Usimshuhudie jirani yako uongo. Usiitamani nyumba ya jirani yako, usimtamani mke wa jirani yako; wala mtumwa wake, wala mjakazi wake, wala ng’ombe wake, wala punda wake, wala cho chote alicho nacho jirani yako.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab. 19:8-11Bwana, unayo maneno ya uzima wa milele.
Sheria ya Bwana ni kamilifu huiburudisha nafsi
Ushuhuda wa Bwana ni amini humtia mjinga hekima.
K. Bwana, unayo maneno ya uzima wa milele.
Maagizo ya Bwana ni adili, huufurahisha moyo,
Amri ya Bwana ni safi, huyatia macho nuru.
K. Bwana, unayo maneno ya uzima wa milele.
Kicho cha Bwana ni kitakatifu, kinadumu milele.
hukumu za Bwana ni kweli, zina haki kabisa.
K. Bwana, unayo maneno ya uzima wa milele.
Ni za kutamanika kuliko dhahabu,
kuliko wingi wa dhahabu safi.
Nazo ni tamu kuliko asali, kuliko sega la asali.
K. Bwana, unayo maneno ya uzima wa milele.
Shangilio la Injili
Mt. 4:4Mtu hataishi kwa mkate tu,
ila kwa kila neno litokalo
katika kinywa cha Mungu
Aleluya.
Injili
Mt. 13:18-23Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni