Jumatano ya 10 ya Mwaka
· Mwaka B · Juma la 2 la Zaburi
Somo la Kwanza
2Kor. 3:4 – 11Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab. 99:5 – 9Bwana, Mungu wetu, ndiye mtakatifu.
Mtukuzeni Bwana, Mungu wetu;
Sujuduni penye kiti cha miguu yake;
Ndiye mtakatifu.
K. Bwana, Mungu wetu, ndiye mtakatifu.
Musa na Haruni miongoni mwa makuhani wake,
Na Samweli miongoni mwao waliitiao jina lake,
Walipomwita Bwana aliwaitikia.
K. Bwana, Mungu wetu, ndiye mtakatifu.
Katika nguzo ya wingu alikuwa akisema nao.
Walishika shuhuda zake na amri aliyowapa.
K. Bwana, Mungu wetu, ndiye mtakatifu.
Ee Bwana, Mungu wetu, ndiwe uliyewajibu;
Ulikuwa kwao Mungu mwenye kusamehe
Ingawa uliwapatiliza matendo yao.
K. Bwana, Mungu wetu, ndiye mtakatifu.
Mtukuzeni Bwana, Mungu wetu;
Sujuduni mkiukabili mlima wake mtakatifu;
Maana Bwana, Mungu wetu, ndiye mtakatifu.
K. Bwana, Mungu wetu, ndiye mtakatifu.
Shangilio la Injili
Zab. 119:135Umwangazie mtumishi wako uso wako, na kunifundisha amri zako.
Aleluya.
Injili
Mt. 5:17-19Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni