Alhamisi ya 7 ya Pasaka
· Mwaka B · Juma la 3 la Zaburi
Somo la Kwanza
Mdo 22:30; 23:6-11Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 16:1-2, 7-11Mungu unihifadhi mimi, Kwa maana nakukimbilia Wewe.
Mungu, unihifadhi mimi,
Kwa maana nakukimbilia Wewe.
Nimemwambia Bwana, Ndiwe Bwana wangu;
Sina wema ila utokao kwako.
K. Mungu unihifadhi mimi, Kwa maana nakukimbilia Wewe.
Nitamhimidi Bwana aliyenipa shauri,
Naam, mtima wangu umenifundisha usiku.
Nimemweka Bwana mbele yangu daima,
Kwa kuwa yuko kuumeni kwangu, sitaondoshwa.
K. Mungu unihifadhi mimi, Kwa maana nakukimbilia Wewe.
Kwa hiyo moyo wangu unafurahi,
Nao utukufu wangu unashangilia,
Naam, mwili wangu nao utakaa kwa kutumaini.
Maana hutakuachia kuzimu nafsi yangu,
Wala hutamtoa mtakatifu wako aone uharibifu.
K. Mungu unihifadhi mimi, Kwa maana nakukimbilia Wewe.
Utanijulisha njia ya uzima;
Mbele za uso wako ziko furaha tele;
Na katika mkono wako wa kuume Mna mema ya milele.
K. Mungu unihifadhi mimi, Kwa maana nakukimbilia Wewe.
Shangilio la Injili
Yn 16:28Nalitoka kwa Baba, nami nimekuja hapa ulimwenguni; tena naucha ulimwengu, na kwenda kwa Baba.
Aleluya.
Injili
Yn 17:20-26Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni