Jumamosi ya 1 ya Kwaresima
· Mwaka B · Juma la 1 la Zaburi
Somo la Kwanza
Kumb 26:16-19Umemwungama Bwana leo, kuwa ndiye Mungu wako, na kuwa yakupasa kutembea katika njia zake, na kushika amri zake na maagizo yake, na hukumu zake, na kusikiza sauti yake; naye Bwana amekuungama hivi leo kuwa taifa iliyotengwa iwe yake yeye, kama alivyokuahidi, na kuwa yakupasa kushika maagizo yake yote; na kuwa atakutukuza juu ya mataifa yote aliyoyafanya kwa sifa, na jina na heshima, nawe upate kuwa taifa takatifu kwa Bwana Mungu wako, kama alivyosema.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 119:1-2, 4-5, 7-8Heri walio kamili njia zao, Waendao katika sheria ya Bwana.
Heri walio kamili njia zao,
Waendao katika sheria ya Bwana.
Heri wazitiio shuhuda zake,
Wamtafutao kwa moyo wote.
K. Heri walio kamili njia zao, Waendao katika sheria ya Bwana.
Wewe umetuamuru mausia yako,
Ili sisi tuyatii sana.
Ningependa njia zangu ziwe thabiti,
Nizitii amri zako.
K. Heri walio kamili njia zao, Waendao katika sheria ya Bwana.
Nitakushukuru kwa unyofu wa moyo,
Nikiisha kujifunza hukumu za haki yako.
Nitazitii amri zako,
Usiniache kabisa.
K. Heri walio kamili njia zao, Waendao katika sheria ya Bwana.
Shangilio la Injili
Amo 5:14Injili
Mt 5:43-48Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni