Alhamisi ya 1 ya Mwaka
· Mwaka B · Juma la 1 la Zaburi
Somo la Kwanza
Ebr 3:7–14Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 95:6–11Ingekuwa heri leo msikie sauti yake! Msifanye migumu mioyo yenu.
Njoni, tuabudu, tusujudu,
Tupige magoti mbele za Bwana aliyetuumba.
Kwa maana ndiye Mungu wetu,
Na sisi tu watu wa malisho yake,
Na kondoo za mkono wake.
K. Ingekuwa heri leo msikie sauti yake! Msifanye migumu mioyo yenu.
Ingekuwa heri leo msikie sauti yake!
Msifanye migumu mioyo yenu,
Kama vile huko Meriba, kama siku ya Masa jangwani.
Hapo waliponijaribu baba zenu,
Wakanipima wakayaona matendo yangu.
K. Ingekuwa heri leo msikie sauti yake! Msifanye migumu mioyo yenu.
Miaka arobaini nalihuzunika na kizazi kile,
Nikasema, Hao ni watu waliopotoka mioyo,
Hawakuzijua njia zangu.
Nikaapa kwa hasira yangu
Wasiingie rahani mwangu.
K. Ingekuwa heri leo msikie sauti yake! Msifanye migumu mioyo yenu.
Shangilio la Injili
Mt 11:25Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu nan chi, kwa kuw amambo haya uliwaficha wenye hekima na akili, ukawafunulia watoto wachanga.
Aleluya.
Injili
Mk 1:40-45Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni