Alhamisi ya Mwaka
· Mwaka C
Somo la Kwanza
Yer 2:1-3, 7-8, 12-13Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 36:5-10Kwako Bwana iko chemchemi ya uzima.
Ee Bwana, fadhili zako zafika hata mbinguni, Uaminifu wako hata mawinguni.
Haki yako ni kama milima ya Mungu, Hukumu zako ni vilindi vikuu.
K. Kwako Bwana iko chemchemi ya uzima.
Ee Mungu, jinsi zilivyo na thamani fadhili zako! Wanadamu huukimbilia uvuli wa mbawa zako.
Watashibishwa kwa unono wa nyumba yako, Nawe utawanywesha mto wa furaha zako.
K. Kwako Bwana iko chemchemi ya uzima.
Maana kwako Wewe iko chemchemi ya uzima, Katika nuru yako tutaona nuru.
Uwadumishie wakujuao fadhili zako, Na wanyofu wa moyo uaminifu wako.
K. Kwako Bwana iko chemchemi ya uzima.
Shangilio la Injili
Mt 11:25Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa mambo haya uliwaficha wenye hekima na akili, ukawafunulia watoto wachanga.
Aleluya
Injili
Mt 13:10-17Maana mioyo ya watu hawa imekuwa mizito, Na kwa masikio yao hawasikii vema, Na macho yao wameyafumba; Wasije wakaona kwa macho yao, Wakasikia kwa masikio yao, Wakaelewa kwa mioyo yao, Wakaongoka, nikawaponya. Lakini, heri macho yenu, kwa kuwa yanaona; na masikio yenu, kwa kuwa yanasikia. Kwa maana, amin, nawaambia, Manabii wengi na wenye haki walitamani kuyaona mnayoyaona ninyi, wasiyaone; na kuyasikia mnayoyasikia ninyi, wasiyasikie.
Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni