Dominika ya 1 ya Majilio
· Mwaka B · Juma la 1 la Zaburi
Somo la Kwanza
Isa 63:16-17; 64:1, 4-8Wwe wamlaki yeye afurahiaye yaliyo haki na kuyatenda, watu wale wakukumbukao katika njia zako; tazama, ulikuwa na hasira, nasi tulitenda dhambi; tumekuwa katika mambo haya muda mwingi; nasi, je! Tukaokolewa? Kwa maana sisi sote tumekuwa kama mtu aliye mchafu, na matendo yetu yote ya haki yamekuwa kama nguo iliyotiwa unajisi; sisi sote twanyauka kama jani, na maovu yetu yatuondoa, kama upepo uondoavyo. Tena hapana aliitiaye jina lako, ajitahidiye akushike; kwa kuwa umetuficha uso wako, nawe umetukomesha kwa njia ya maovu yetu. Lakini sasa, Ee Bwana, wewe u baba yetu; sisi tu udongo, nawe u mfinyanzi wetu; sisi sote tu kazi ya mikono yako.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 80:1-2, 14-15, 17-18Ee Mungu, uturudishe, uangazishe uso wako nasi tutaokoka.
Wewe uchungaye Israeli usikie,
Wewe uketiye juu ya makerubi, utoe nuru.
Uziamshe nguvu zako.
Uje, utuokoe.
K. Ee Mungu, uturudishe, uangazishe uso wako nasi tutaokoka.
Ee Mungu wa majeshi, tunakusihi, urudi,
Utazame toka juu uone, uujilie mzabibu huu.
Na mche ule ulioupanda
Kwa mkono wako wa kuume;
Na tawi lile ulilolifanya
Kuwa imara kwa nafsi yako.
K. Ee Mungu, uturudishe, uangazishe uso wako nasi tutaokoka.
Mkono wako na uwe juu yake
Mtu wa mkono wako wa kuume;
Juu ya mwanadamu uliyemfanya
Kuwa imara kwa nafsi yako;
Basi hatutakuacha kwa kurudi nyuma;
Utuhuishe nasi tutaliitia jina lako.
K. Ee Mungu, uturudishe, uangazishe uso wako nasi tutaokoka.
Somo la Pili
1Kor 1:3-9Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Shangilio la Injili
Zab 85:7Ee Bwana utuonyeshe rehema zako utupe wokovu wako,
Aleluya.
Injili
Mk 13:33-37Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni