Kumbukumbu ya Kutolewa Bikira Maria Hekaluni
· Mwaka A · Juma la 1 la Zaburi
Somo la Kwanza
Ufu 11:4–12Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 144:1–2, 9–10Ahimidiwe Bwana, mwamba wangu.
Ahimidiwe Bwana, mwamba wangu,
Anifundishaye mikono yangu vita,
Vidole vyangu kupigana.
K. Ahimidiwe Bwana, mwamba wangu.
Mhisani wangu na boma langu,
Ngome yangu na mwokozi wangu,
Ngao yangu niliyemkimbilia,
Huwatiisha watu wangu chini yangu.
K. Ahimidiwe Bwana, mwamba wangu.
Ee Mungu, nitakuimbia wimbo mpya,
Kwa kinanda chenye nyuzi kumi nitakuimbia.
Awapaye wafalme wokovu,
Amwokoa Daudi, mtumishi wake, na upanga wa uovu.
K. Ahimidiwe Bwana, mwamba wangu.
Shangilio la Injili
Kol 3:16–17Neno la Kristo likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkimshukuru Mungu Baba kwa yeye.
Aleluya.
Injili
Lk 20:27-40Yesu akawaambia, Wana wa ulimwengu huu huoa na kuolewa; lakini, wale wahesabiwao kuwa wamestahili kuupata ulimwengu ule, na kule kufufuka katika wafu, hawaoi wala hawaolewi; wala hawawezi kufa tena; kwa sababu huwa sawasawa na malaika, nao ni wana wa Mungu, kwa vile walivyo wana wa ufufuo. Lakini, ya kuwa wafu hufufuliwa, hata na Musa alionyesha katika sura ya Kijiti, hapo alipomtaja Bwana kuwa ni Mungu wa Ibrahimu, na Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo. Naye si Mungu wa wafu, bali wa walio hai; kwa kuwa wote huishi kwake. Waandishi wengine wakajibu wakamwambia, Mwalimu, umesema vema; wala hawakuthubutu kumwuliza neno baada ya hayo.
Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni