Sherehe ya Watakatifu Wote
· Mwaka A
Somo la Kwanza
Ufu 7:2-4,9-14Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 24:1-6Hiki ndicho kizazi cha wakutafutao, Ee Bwana.
Nchi na vyote viijazavyo ni mali ya Bwana,
Dunia na wote wakaao ndani yake.
Maana ameiweka misingi yake juu ya bahari,
Na juu ya mito ya maji aliithibitisha.
K. Hiki ndicho kizazi cha wakutafutao, Ee Bwana.
Ni nani atakayepanda katika mlima wa Bwana?
Ni nani atakayesimama katika patakatifu pake?
Mtu aliye na mikono safi na moyo mweupe,
Asiyeiinua nafsi yake kwa ubatili.
K. Hiki ndicho kizazi cha wakutafutao, Ee Bwana.
Atapokea Baraka kwa Bwana,
Na haki kwa Mungu wa wokovu wake.
Hiki ndicho kizazi cha wamtafutao,
Wakutafutao uso wako, Ee Mungu wa Yakobo.
K. Hiki ndicho kizazi cha wakutafutao, Ee Bwana.
Somo la Pili
1Yoh 3:1-3Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Shangilio la Injili
Mt 11:28Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa
na mizigo, nami nitawapumzisha, asema Bwana.
Aleluya.
Injili
Mt 5:1-12Heri walio maskini wa roho; Maana ufalme wa mbinguni ni wao.
Heri wenye huzuni; Maana hao watafarijika.
Heri wenye upole; Maana hao watairithi nchi.
Heri wenye njaa na kiu ya haki; Maana hao watashibishwa.
Heri wenye rehema; Maana hao watapata rehema.
Heri wenye moyo safi; Maana hao watamwona Mungu.
Heri wapatanishi; Maana hao wataitwa wana wa Mungu.
Heri wenye kuudhiwa kwa ajili ya haki; Maana ufalme wa mbinguni ni wao.
Heri ninyi watakapowashutumu na kuwaudhi na kuwanenea kila neno baya kwa uongo, kwa ajili yangu. Furahini, na kushangilia; kwa kuwa thawabu yenu ni kubwa mbinguni; kwa maana ndivyo walivyowaudhi manabii waliokuwa kabla yenu.
Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (1)
edwin msekalile · 1 Novemba 2020
Amina nashukuru kwa neno