Alhamisi ya 15 Mwaka
· Mwaka C
Somo la Kwanza
Isa 26: 7-9, 12, 16-19Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 102:12-20Toka mbinguni Bwana ameangalia nchi.
Bali Wewe, Bwana utaketi ukimiliki milele, Na kumbukumbu lako kizazi hata kizazi.
Wewe mwenyewe utasimama, Na kuirehemu Sayuni, Kwa maana ndio wakati wa kuihurumia,
Maana watumishi wako wameyaridhia mawe yake, Na kuyaonea huruma mavumbi yake.
K. Toka mbinguni Bwana ameangalia nchi.
Kisha mataifa wataliogopa jina la Bwana, Na wafalme wote wa dunia utukufu wako;
Bwana atakapokuwa ameijenga Sayuni, Atakapoonekana katika utukufu wake,
Atakapoyaelekea maombi yake aliye mkiwa, Asiyadharau maombi yao.
K. Toka mbinguni Bwana ameangalia nchi.
Kizazi kitakachokuja kitaandikiwa hayo, Na watu watakaoumbwa watamsifu Bwana.
Maana ametazama toka patakatifu pake pa juu, Toka mbinguni Bwana ameiangalia nchi,
Ili akusikie kuugua kwake aliyefungwa, Na kuwafungua walioandikiwa kufa.
K. Toka mbinguni Bwana ameangalia nchi.
Shangilio la Injili
Mt 11:28Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.
Aleluya
Injili
Mt 11:28-30Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni