Alhamisi ya 25 ya Mwaka
· Mwaka A · Juma la 1 la Zaburi
Somo la Kwanza
Mhu 1:1–11Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 90:3–6, 12–14, 17Wewe, Bwana, umekuwa makao yetu, kizazi baada ya kizazi.
Wamrudisha mtu mavumbini,
Usemapo, Rudini, enyi wanadamu.
Maana miaka elfu machoni pako
Ni kama siku ya jana ikiisha kupita,
Na kama kesha la usiku.
K. Wewe, Bwana, umekuwa makao yetu, kizazi baada ya kizazi.
Wawagharikisha, huwa kama usingizi,
Asubuhi huwa kama majani yameayo.
Asubuhi yachipuka na kumea,
Jioni yakatika na kukauka.
K. Wewe, Bwana, umekuwa makao yetu, kizazi baada ya kizazi.
Basi, utujulishe kuzihesabu siku zetu,
Tujipatie moyo wa hekima.
Ee Bwana, urudi, hata lini?
Uwahurumie watumishi wako.
K. Wewe, Bwana, umekuwa makao yetu, kizazi baada ya kizazi.
Utushibishe asubuhi kwa fadhili zako,
Nasi tutashangilia na kufurahi siku zetu zote.
Na uzuri wa Bwana, Mungu wetu, uwe juu yetu,
Na kazi ya mikono yetu utufanyie thabiti.
K. Wewe, Bwana, umekuwa makao yetu, kizazi baada ya kizazi.
Shangilio la Injili
Zab 27:11Ee Bwana, unifundihse njia yako, na kuniongoza katika njia iliyonyoka.
Aleluya.
Injili
Lk 9:7–9Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni