Kumbuumbu ya Mt. Gregori Mkuu, Papa na Mwalimu wa
· Mwaka A · Juma la 2 la Zaburi
Somo la Kwanza
1Kor 3:18–23Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 24:1–6Nchi na vyote viijazavyo ni mali ya Bwana.
Nchi na vyote viijazavyo ni mali ya Bwana,
Dunia na wote wakaao ndani yake.
Maana ameiweka misingi yake juu ya bahari,
Na juu ya mito ya maji aliithibitisha.
K. Nchi na vyote viijazavyo ni mali ya Bwana.
Ni nani atakayepanda katika mlima wa Bwana?
Ni nani atakayesimama katika patakatifu pake?
Mtu aliye na mikono safi na moyo mweupe,
Asiyeiinua nafsi yake kwa ubatili,
Wala hakuapa kwa hila.
K. Nchi na vyote viijazavyo ni mali ya Bwana.
Atapokea Baraka kwa Bwana,
Na haki kwa Mungu wa wokovu wake.
Hiki ndicho kizazi cha wamtafutao,
Wakutafutao uso wako, Ee Mungu wa Yakobo.
K. Nchi na vyote viijazavyo ni mali ya Bwana.
Shangilio la Injili
1Thes 2:13Lipokeeni neno la Mungu, siyo kama neno la wanadamu, bali kama neno la Mungu.
Aleluya.
Injili
Lk 5:1–11Simoni Petro alipona hayo, alianguka magotini pa yesu, akisema, Ondoka kwangu, kwa kuwa mimi ni mtu mwenye dhambi, Bwana. Maana alishikwa na ushangao, yeye na wote waliokuwa pamoja naye, kwa sababu ya wingi wa samaki walaioupata; na kadhalika Yakobo na Yohane, wana wa Zebedayo, waliokuwa washirika wa Simoni. Yesu akamwambia Simoni, Usiogope, tangu sasa utakuwa ukivua watu. Hata walipokwisha kuviegesha pwani vyombo vyao, wakaacha vyote wakamfuata.
Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (2)
Marie Melina · 4 Septemba 2020
Please weka uwezekajo wa ku search masomo for the coming days siyo previous days only. Some of us want to know the readings for the next day.
Marie Melina · 4 Septemba 2020
Please weka uwezekajo wa ku search masomo for the coming days siyo previous days only. Some of us want to know the readings for the next day.