Jumatano ya 18 ya Mwaka
· Mwaka A · Juma la 2 la Zaburi
Somo la Kwanza
Yer 31:1–7Maana Bwana asema hivi, Mwimbieni Yakobo kwa furaha, mkampigie kelele mkuu wa mataifa, tangazeni, sifuni, mkasema, Ee Bwana, uwaokoe watu wako mabaki ya Israeli.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Yer 31:10–13Bwana atatulinda kama mchungaji alindavyo kundi lake.
Lisikieni neno la Bwana,
Enyi mataifa, litangazeni visiwani mbali,
Mkaseme Aliyemtawanya Israeli atamkusanya,
Na kumlinda, kama mchungaji alindavyo kundi lake.
Kwa maana Bwana amemweka huru Yakobo,
Amemkomboa mkononi mwake
Aliyekuwa hodari kuliko yeye.
K. Bwana atatulinda kama mchungaji alindavyo kundi lake.
Nao watakuja, na kuimba katika mlima Sayuni,
Wataukimbilia wema wa Bwana, nafaka, na divai;
Na mafuta, na wachanga wa kondoo na wa ng’ombe
Na roho zao zitakuwa kama bustani iliyotiwa maji;
Wala hawatauzunika tena kabisa.
K. Bwana atatulinda kama mchungaji alindavyo kundi lake.
Ndipo bikira atafurahi katika kucheza,
Na vijana na wazee pamoja;
Maana nitageuza masikitiko yao kuwa furaha,
Nami nitawafariji,
Na kuwafurahisha waache huzuni zao.
K. Bwana atatulinda kama mchungaji alindavyo kundi lake.
Shangilio la Injili
Zab 119:105Neno lako ni taa ya miguu yangu, na mwanga wa njia yangu.
Aleluya.
Injili
Mt 15:21–28Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni