Jumamosi ya 12 ya Mwaka
· Mwaka A · Juma la 4 la Zaburi
Somo la Kwanza
Omb 2:2, 10–14, 18–19Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 74:1–7, 20–21Usiusahau milele uhai wa watu wako walioonewa.
Ee Mungu, mbona umetutupa milele?
Kwa nini hasira yako inatoka moshi
Juu ya kondoo wa malisho yako?
Ulikumbuke kusanyiko lako,
Ulilolinunua zamani.
Ulilolikomboa liwe kabila la urithi wako,
Mlima Sayuni ulioufanya maskani yako.
K. Usiusahau milele uhai wa watu wako walioonewa.
Upainulie miguu yako palipoharibika milele;
Adui ameufanya kila ubaya katika patakatifu.
Watesi wako wamenguruma kati ya kusanyiko lako;
Wameweka bendera zao ziwe alama.
K. Usiusahau milele uhai wa watu wako walioonewa.
Wanaonekana kama watu wainuao mashoka,
Waikate miti ya msituni.
Na sasa nakishi yake yote pia
Wanaivunjavunja kwa mashoka na nyundo.
Wamepatia moto patakatifu pako;
Wamelinajisi kao la jina lako hata chini.
K. Usiusahau milele uhai wa watu wako walioonewa.
Ulitafakari agano;
Maana mahali penye giza katika nchi
Pamejaa makao ya kukatili.
Aliyeonewa asirejee ametiwa haya,
Mnyonge na mhitaji na walisifu jina lako.
K. Usiusahau milele uhai wa watu wako walioonewa.
Shangilio la Injili
Yn 8:12Mimi ndimi nuru ya ulimwengu, asema Bwana, yeye anifuataye hatakwenda gizani kamwe, bali atakuwa na nuru ya uzima.
Aleluya.
Injili
Mt 8:5–17Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni