Kumbukumbu ya Mt. Barnaba, Mtume.
· Mwaka A
Somo la Kwanza
Mdo 11:21-26, 13:1-3Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 98:1-6Bwana ameufunua wokovu wake machoni pa mataifa.
Mwimbieni Bwana wimbo mpya,
Kwa maana ametenda mambo ya ajabu.
Mkono wa kuume wake mwenyewe,
Mkono wake mtakatifu umemtendea wokovu.
K. Bwana ameufunua wokovu wake machoni pa mataifa.
Bwana ameufunua wokovu wake,
Machoni pa mataifa ameidhihirisha haki yake.
Amezikumbuka rehema zake,
Na uaminifu wake kwa nyumba ya Israeli.
K. Bwana ameufunua wokovu wake machoni pa mataifa.
Miisho yote ya dunia imeuona
Wokovu wa Mungu wetu.
Mshangilieni Bwana, nchi yote,
Inueni sauti, imbeni kwa furaha, imbeni zaburi.
K. Bwana ameufunua wokovu wake machoni pa mataifa.
Mwimbieni Bwana zaburi kwa kinubi,
Kwa kinubi na sauti ya zaburi.
Kwa panda na sauti ya baragumu.
Shangilieni mbele za Mfalme, Bwana.
K. Bwana ameufunua wokovu wake machoni pa mataifa.
Shangilio la Injili
ShangilioEe Mungu, tunakusifu, tunakukiri kuwa Bwana. Jamii tukufu ya mitume inakusifu.
Aleluya.
Injili
Mt 10:7-13Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni