Jumatatu ya 7 ya Mwaka
· Mwaka A · Juma la 3 la Zaburi
Somo la Kwanza
Mdo 19:1-8Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 68:1-6Enyi falme za dunia, mwimbieni Mungu
Mungu huondoka, adui zake wakatawanyika,
Nao wamchukiao huukimbia uso wake.
Kama moshi upeperushwavyo,
Ndivyo uwapeperushavyo wao;
Kama nta iyeyukavyo mbele ya moto,
Ndivyo waovu wapoteavyo usoni pa Mungu.
K. Enyi falme za dunia, mwimbieni Mungu
Bali wenye haki hufurahi,
Na kuushangilia uso wa Mungu,
Naam, hupiga kelele kwa furaha.
Mwimbieni Mungu, lisifuni jina lake,
Shangilieni mbele zake.
K. Enyi falme za dunia, mwimbieni Mungu
Baba wa yatima na mwamuzi wa wajane,
Mungu katika kao lake takatifu.
Mungu huwakalisha wapweke nyumbani;
Huwatoa wafungwa wakae hali ya kufanikiwa;
Bali wakaidi hukaa katika nchi kavu.
K. Enyi falme za dunia, mwimbieni Mungu
Shangilio la Injili
Mt 28:19, 20Enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mimi nipo pamoja nanyi sikuzote, hata ukamilifu wa dahari.
Aleluya.
Injili
Yn 16:29-33Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni