Jumatatu ya 13 ya mwaka
· Mwaka C
Somo la Kwanza
Amo 2:6-10, 13-16Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 50:16-23Una nini wewe kuitangaza sheria yangu, Na kuliweka agano langu kinywani mwako?
Maana wewe umechukia maonyo, Na kuyatupa maneno yangu nyuma yako.
(K)Yafahamuni hayo, ninyi mnaomsahau Mungu.
Ulipomwona mwivi ulikuwa radhi naye, Ukashirikiana na wazinzi.
Umekiachia kinywa chako kinene mabaya, Na ulimi wako watunga hila.
(K)Yafahamuni hayo, ninyi mnaomsahau Mungu.
Umekaa na kumsengenya ndugu yako, Na mwana wa mama yako umemsingizia.
Ndivyo ulivyofanya, nami nikanyamaza; Ukadhani ya kuwa Mimi ni kama wewe.
Walakini nitakukemea; Nitayapanga hayo mbele ya macho yako.
(K)Yafahamuni hayo, ninyi mnaomsahau Mungu.
Yafahamuni hayo, Ninyi mnaomsahau Mungu, Nisije nikawararueni,
Asipatikane mwenye kuwaponya.
Atoaye dhabihu za kushukuru, Ndiye anayenitukuza.
Naye autengenezaye mwenendo wake, Nitamwonyesha wokovu wa Mungu.
(K)Yafahamuni hayo, ninyi mnaomsahau Mungu.
Shangilio la Injili
Zab 95:8Ikiwa leo mwasikia sauti yake, Msifanye migumu mioyo yenu;
Aleluya
Injili
Mt 8:18-22Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni