Dominika ya 2 ya Pasaka
· Mwaka A · Juma la 2 la Zaburi
Somo la Kwanza
Mdo 2:42–47Kila mtu akaingiwa na hofu; ajabu nyingi na ishara zikafanywa na mitume.
Na wote walioamini walikuwa mahali pamoja, na kuwa na vitu vyote shirika, wakiuza mali zao, na vitu vyao walivyokuwa navyo, na kuwagawia watu wote kama kila mtu alivyokuwa na haja.
Na siku zote kwa moyo mmoja walidumu ndani ya hekalu, walimega mkate nyumba kwa nyumba, na kushiriki chakula chao kwa furaha na kwa moyo mweupe, wakimsifu Mungu, na kuwapendeza watu wote. Bwana akalizidisha kanisa kila siku kwa wale waliokuwa wakiokolewa.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 11:2–4, 13–15, 22–24Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema, kwa maana fadhili zake ni za milele.
Israeli na aseme sasa,
Ya kwamba fadhili zake ni za milele.
Mlango wa Haruni na waseme sasa,
Ya kwamba fadhili zake ni za milele.
K. Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema, kwa maana fadhili zake ni za milele.
Ulinisukuma sana ili nianguke;
Lakini Bwana akanisaidia.
Bwana ni nguvu zangu na wimbo wangu,
Naye amekuwa wokovu wangu.
Sauti ya furaha na wokovu
Imo hemani mwao wenye haki.
K. Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema, kwa maana fadhili zake ni za milele.
Jiwe walilolikataa waashi
Limekuwa jiwe kuu la pembeni.
Neno hili limetoka kwa Bwana,
Nalo ni ajabu machoni petu.
Siku hii ndiyo aliyoifanya Bwana,
Tutaishangilia na kuifurahia.
K. Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema, kwa maana fadhili zake ni za milele.
Somo la Pili
1Pet 1:3–9Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Shangilio la Injili
Yn 20:29Yesu akamwambia, Wewe, kwa kuwa umeniona, umesadfiki; wa heri wale wasioona, wakasadiki.
Aleluya.
Injili
Yn 20:19–31Walakini mmoja wa wale Thenashara, Tomaso, aitwaye Pacha, hakuwako pamoja nao alipokuja Yesu. Basi wanafunzi wengine wakamwambia, Tumemwona Bwana. Akawaambia, Mimi nisipoziona mikononi mwake kovu za misumari, na kutia kidole changu katika mahali pa misumari, na kutia mkono wangu katika ubavu wake, mimi sisadiki hata kidogo. Basi, baada ya siku nane, wanafunzi wake walikuwamo ndani tena, na Tomaso pamoja nao. Akaja Yesu, na milango imefungwa, akasimama katikati akasema, Amani iwe kwenu. Kisha akamwambia Tomaso, Lete hapa kole chako, uitazame mikono yangu; ulete na mkono wako uutie ubavuni mwangu; wala usiwe asiyeamini, bali aaminiye. Tomaso akajibu, akamwambia, Bwana wangu na Mungu wangu! Yesu akamwambia, Wewe, kwa kuwa umeniona, umesadiki; wa heri wale wasioona, wakasadiki. Basi kuna ishara nyingine nyingi alizozifanya Yesu mbele ya wanafunzi wake, zisizoandikwa katika kitabu hiki. Lakini hizi zimeandikwa; ili mpate kuamini ya kwamba Yesu ndiye Kristo, Mwana wa Mungu; na kwa kuamini na uzima kwa jina lake.
Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni