Alhamisi baada ya Majivu
· Mwaka A · Juma la 4 la Zaburi
Somo la Kwanza
Kum 30:15-20Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 1:1-4, 6Heri mtu aliyemfanya Bwana kuwa tumaini lake.
Heri mtu yule asiyekwenda
Katika shauri la wasio haki;
Wala hakusimama katika njia ya wakosaji;
Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha.
Bali sheria ya Bwana ndiyo impendezayo,
Na sheria yake huitafakari mchana na usiku.
K. Heri mtu aliyemfanya Bwana kuwa tumaini lake.
Naye atakuwa kama mti ulipopandwa
Kandokando ya vijito vya maji,
Uzaao matunda yake kwa majira yake,
Wala jani lake halinyauki;
Na kila alitendalo litafanikiwa.
K. Heri mtu aliyemfanya Bwana kuwa tumaini lake.
Sivyo walivyo wasio haki;
Hao ni kama makapi yapeperushayo na upepo.
Kwa kuwa Bwana anaijua njia ya wenye haki,
Bali njia ya wasio haki itapotea.
K. Heri mtu aliyemfanya Bwana kuwa tumaini lake.
Shangilio la Injili
Zab 130:5Injili
Lk 9:22-25Akawaambia wote, Mtu yeyote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake kila siku, anifuate. Kwa kuwa mtu atakaye kuiponya nafsi yake ataiangamiza, na mtu atakayeiangamiza nafsi yake kwa ajili yangu ndiye atakayeisalimisha. Kwa kuwa yamfaa nini mtu kuupata ulimwengu wote, kama akijiangamiza, na kujipoteza mwenyewe?
Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni