Sikukuu ya Mt. Stefano
· Mwaka A
Somo la Kwanza
Mdo 6:8-10, 7:54-60Lakini yeye akijaa Roho Mtakatifu, akakaza macho yake, akitazama mbinguni, akauona, utukufu wa Mungu, na Yesu akisimama upande wa mkono wa kuume wa Mungu. Akasema, Tazama, naona mbingu zimefunguka, na Mwana wa Adamu amesimama mkono wa kuume wa Mungu. Wakapiga kelele kwa sauti kuu, wakaziba masikio yao wakamrukia kwa nia moja, wakamtoa nje ya mji, wakampiga kwa mawe. Nao mashahidi wakaweka nguo zao miguuni pa kijana mmoja aliyeitwa Sauli. Wakampiga kwa mawe Stefano, naye akiomba, akisema, Bwana Yesu, pokea roho yangu. Akapiga magoti, akalia kwa sauti kuu, Bwana, usiwahesabie dhambi hii. Akiisha kusema haya akalala. Na Sauli alikuwa akiona vema kwa kuuawa kwake.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 31:2-3, 5-7, 16, 20Mikononi mwako, naiweka roho yangu, Ee Bwana.
Uwe kwangu mwamba wa nguvu,
Nyumba yenye maboma ya kuniokoa.
Ndiwe genge langu na ngome yangu;
Kwa ajili ya jina lako uniongoze, unichunge.
K. Mikononi mwako, naiweka roho yangu, Ee Bwana.
Mikononi mwako naiweka roho yangu;
Umenikomboa, Ee Bwana, Mungu wa kweli.
Bali mimi namtumaini Bwana.
Na nishangilie, nizifurahie fadhili zako.
K. Mikononi mwako, naiweka roho yangu, Ee Bwana.
Umwangaze mtumishi wako
Kwa nuru ya uso wako;
Uniokoe kwa ajili ya fadhili zako.
K. Mikononi mwako, naiweka roho yangu, Ee Bwana.
Shangilio la Injili
ShangilioAbarikiwe yeye ajaye kwa jina la Bwana; Bwana ndiye aliyetupa nuru.
Aleluya.
Injili
Mt 10:17-22Na ndugu atamsaliti nduguye ili auawe, na baba atamsaliti mwana, na wana watawainukia wazazi wao, na kuwasafisha. Nanyi mtakuwa mkichukiwa na watu wote kwa ajili ya jina langu; lakini mwenye kuvumilia hata mwisho, ndiye atakayeokoka.
Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni