Jumatatu ya 1 ya Majilio
· Mwaka A · Juma la 1 la Zaburi
Somo la Kwanza
Isa 4:2-6Hapo Bwana atakapokuwa ameuosha uchafu wa hao binti za Sayuni na kuisafisha damu ya Yerusalemu kati yake. kwa roho ya hukumu na kwa roho ya kuteketeza. Tena juu ya makao yote ya mlima Sayuni. na juu ya makusanyiko yake. Bwana ata umba wingu na moshi wakati wa mchana na mwangaza wa miali ya moto wakati wa usiku; kwa maana juu ya utukufu wote itatandazwa sitara. Kisha kutakuwa na hema kuwa uvuli wakati wa mchana kwa sababu ya hari, na kuwa mahali pa kukimbilia na kujificha wakati wa tufani na mvua.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 122:1-4, 8, 9Nalifurahi waliponiambia, Na twende nyumbani kwa Bwana.
Nalifurahi waliponiarabia,
Na twende nyumbani kwa Bwana.
Miguu yetu imesimama
Ndani ya malango yako, Ee Yerusalemu.
K. Nalifurahi waliponiambia, Na twende nyumbani kwa Bwana.
Ee Yerusalemu ulivejengwa Kama mji ulioshikamana,
Huko ndiko walikopanda kabila Kabila za Bwana.
K. Nalifurahi waliponiambia, Na twende nyumbani kwa Bwana.
Kwa ajili ya ndugu zangu na rafiki zangu Niseme sasa. Amani ikae nawe
Kwa ajili ya nyumba ya Bwana. Mungu wetu Nikutafutie mema.
K. Nalifurahi waliponiambia, Na twende nyumbani kwa Bwana.
Shangilio la Injili
Zab 80:4Ee Bwana, Mungu wa majeshi, hata lini? Utayagadhabikia maombi ya watu wako?
Aleluya.
Injili
Mt 8:1-11Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni