Jumanne ya 10 ya Mwaka
· Mwaka C
Somo la Kwanza
1Fal 17: 7-16Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 4:1-4, 6-7Bwana, utuinulie nuru ya uso wako.
Ee Mungu wa haki yangu, uniitikie niitapo;
Umenifanyizia nafasi wakati wa shida;
Unifadhili na kuisikia sala yangu.
Enyi wanadamu, hata lini utukufu wangu utafedheheka?
Je! Mtapenda ubatili na kutafuta uongo?
K. Bwana, utuinulie nuru ya uso wako.
Bali jueni ya kuwa Bwana amejiteulia mtauwa;
Bwana atasikia nimwitapo.
Mwe na hofu wala msitende dhambi,
Tafakarini vitandani mwenu na kutulia.
K. Bwana, utuinulie nuru ya uso wako.
Nani atakayetuonyesha mema? Bwana,
utuinulie nuru ya uso wako.
Umenitia furaha moyoni mwangu,
Kupita yao wanapozidishiwa nafaka na divai.
K. Bwana, utuinulie nuru ya uso wako.
Shangilio la Injili
Mt 5:16Vivyo hivyo nuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni.
Aleluya
Injili
Mt 5:13-16Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni