Jumatatu ya 26 ya Mwaka
· Mwaka C · Juma la 2 la Zaburi
Somo la Kwanza
Zek 8:1-8Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 102:15-20, 28, 21-22Bwana atakapokuwa ameijenga Sayuni, atakapoonekana katika utukufu wake.
Kisha mataifa wataliogopa jina la Bwana,
Na wafalme wote wa dunia utukufu wako;
Bwana atakapokuwa ameijenga Sayuni,
Atakapoonekana katika utukufu wake,
Atakapoyaelekea maombi yake aliye mkiwa,
Asiyadharau maombi yao.
K. Bwana atakapokuwa ameijenga Sayuni, atakapoonekana katika utukufu wake.
Kizazi kitakachokuja kitaandikiwa hayo,
Na watu watakaoumbwa watamsifu Bwana.
Maana ametazama toka patakatifu pake pa juu,
Toka mbinguni Bwana ameiangalia nchi,
Ili akusikie kuugua kwake aliyefungwa,
Na kuwafungua walioandikiwa kufa.
K. Bwana atakapokuwa ameijenga Sayuni, atakapoonekana katika utukufu wake.
Wana wa watumishi wako watakaa,
Na wazao wao wataimarishwa mbele zako.
Watu walitangaze jina la Bwana katika Sayuni,
Na sifa zake katika Yerusalemu,
Pindi mataifa watapokusanyika pamoja,
Falme nazo ili kumtumikia Bwana.
K. Bwana atakapokuwa ameijenga Sayuni, atakapoonekana katika utukufu wake.
Injili
Lk 9:46-50Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni