Dominika ya 16 ya Mwaka
· Mwaka C · Juma la 4 la Zaburi
Somo la Kwanza
Mwa 18:1-10Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 15Bwana, ni nani atakayekaa katika hema yako
Bwana, ni nani atakayefanya maskani yake
Katika kilima chako kitakatifu?
Ni yeye aendaye kwa ukamilifu,
Na kutenda haki;
Asemaye kweli kwa moyo wake,
Asiyesingizia kwa ulimi wake.
K. Bwana, ni nani atakayekaa katika hema yako
Yeye ambaye hakumtenda mwenziwe mabaya,
Wala hakumsengenya jirani yake.
Machoni pake mtu asiyefaa hudharauliwa,
Bali huwaheshimu wamchao Bwana.
K. Bwana, ni nani atakayekaa katika hema yako
Yeye ambaye hakutoa fedha yake apate kula riba,
Hakutwaa rushwa amwangamize asiye na hatia.
Mtu atendaye mambo hayo
Hataondoshwa milele.
K. Bwana, ni nani atakayekaa katika hema yako
Somo la Pili
Kol 1:24-28Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Shangilio la Injili
Yn 14:23Mtu akinipenda, atalishika neno langu; Na Baba yangu atampenda; Nasi tutakuja kwake.
Aleluya.
Injili
Lk 10:38-42Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (2)
Ernest Gerdath · 21 Julai 2019
Hakika nimejifunza kitu kupitia masomo ya leo
Ernest Gerdath · 21 Julai 2019
Hakika nimejifunza kitu kupitia masomo ya leo