Jumatatu ya 1 ya Mwaka
· Mwaka C · Juma la 1 la Zaburi
Somo la Kwanza
2Kor 1:1-7Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 34:1-8Onjeni muone ya kuwa Bwana yu mwema.
Nitamhimidi Bwana kila wakati,
Sifa zake zi kinywani mwangu daima.
Katika Bwana nafsi yangu itajisifu,
Wanyenyekevu wasikie wakafurahi.
K. Onjeni muone ya kuwa Bwana yu mwema.
Mtukuzeni Bwana pamoja nami,
Na tuliadhimishe jina lake pamoja.
Nalimtafuta Bwana akanijibu,
Akaniponya na hofu zangu zote.
K. Onjeni muone ya kuwa Bwana yu mwema.
Wakamwelekea macho wakatiwa nuru,
Wala nyuso zao hazitaona haya.
Maskini huyu aliita, Bwana akasikia,
Akamwokoa na taabu zake zote.
K. Onjeni muone ya kuwa Bwana yu mwema.
Malaika wa Bwana hufanya kituo,
Akiwazungukia wamchao na kuwaokoa.
Onjeni mwone ya kuwa Bwana yu mwema;
Heri mtu yule anayemtumaini.
K. Onjeni muone ya kuwa Bwana yu mwema.
Injili
Mt 5:1-12Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (1)
jose lucas · 10 Juni 2019
nimependa sana neno na injili ya leo pia namwomba sana mwenyezi Mungu anijaze roho mtakatifu ili niweze kuliishi na kulishika neno lake sku zote katika maisha yangu!Amina!