Kumbukumbu ya Mt. Yosefu Mfanyakazi
· Mwaka C
Somo la Kwanza
Mwa. 1 : 26-2 : 3Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab. 90:2-4, 12-14, 16Kazi ya mikono yetu uithibitishe, Ee Bwana.
Kabla haijazaliwa milima, wala hujaiumba duma,
Na tangu milele hata milele ndiwe Mungu.
K. Kazi ya mikono yetu uithibitishe, Ee Bwana.
Wamrudisha mtu mavumbini,
Usemapo, Rudini, enyi wanadamu.
Maana miaka elfu machoni pako
Ni kama siku ya jana ikiisha kupita,
Na kama kesha la usiku.
K. Kazi ya mikono yetu uithibitishe, Ee Bwana.
Basi, utujulishe kuzihesabu siku zetu,
Tujipatie moyo wa hekima.
Ee Bwana, urudi, hata lini?
Uwahurumie watumishi wako.
K. Kazi ya mikono yetu uithibitishe, Ee Bwana.
Utushibishe asubuhi kwa fadhili zako,
Nasi tutashangilia na kufurahi siku zetu zote.
Matendo yako na yaonekane kwa watumishi wako.
Na adhama yako kwa watoto wako.
K. Kazi ya mikono yetu uithibitishe, Ee Bwana.
Injili
Mt. 13:54-58Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni