Jumanne ya 4 ya Kwaresima
· Mwaka C · Juma la 4 la Zaburi
Somo la Kwanza
Eze. 47:1-9, 12Kisha akapima dhiraa elfu, akanivusha maji yale, maji yakafika mpaka magoti. Kisha akapima dhiraa elfu, akanivusha, maji yakafika mpaka viuno. Kisha akapima dhiraa elfu, yakawa mto nisioweza kuuvuka; maana maji yamezidi, maji ya kuogelea, mto usiovukika. Akaniambia, Mwanadamu, je! Umeona haya? Kisha akanichukua, akanirudisha mpaka ukingo wa mto.
Basi nikiisha kurudi, tazama, kando ya ukingo wa mto ilikuwapo miti mingi sana, upande huu na upande huu. Ndipo akaniambia, Maji haya yanatoka kwenda pande za nchi ya mashariki, nayo yanashuka mpaka Araba, na kuingia katika bahari; maji yatokezwayo yataingia baharini, na maji yake yataponyeka. Tena itakuwa, kila kiumbe hai kisonganacho, kila mahali itakapofika mito hiyo, kitaishi; kutakuwapo wingi mkubwa wa samaki, kwa sababu maji haya yamefika huko; maana maji yale yataponyeka, na kila kitu kitaishi popote utakapofikilia mto huo.
Na karibu na mto, juu ya ukingo wake, upande huu na upande huu, utamea kila mti wa chakula, ambao majani yake hayatanyauka, wala matunda yake hayatatindika kamwe; utatoa matunda mapya kila mwezi, kwa sababu maji yake yanatoka mahali patakatifu; na matunda yake yatakuwa ni chakula; na majani yake yatakuwa ni dawa.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab. 46:1-2, 4-5, 7-8Bwana wa majeshi yu pamoja nasi, Mungu wa Yakobo ni ngome yetu.
Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu,
Msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso.
Kwa hiyo hatutaogopa ijapobadilika nchi,
Ijapotetemeka milima moyoni mwa bahari.
K. Bwana wa majeshi yu pamoja nasi, Mungu wa Yakobo ni ngome yetu.
Kuna mto, vijito vyake vyaufurahisha mji wa Mungu,
Patakatifu pa maskani zake Aliye juu.
Mungu yu katikati yake hautatetemeshwa;
Mungu atausaidia asubuhi na mapema.
K. Bwana wa majeshi yu pamoja nasi, Mungu wa Yakobo ni ngome yetu.
Bwana wa majeshi yu pamoja nasi,
Mungu wa Yakobo ni ngome yetu.
Njoni myatazame matendo ya Bwana,
Jinsi alivyofanya ukiwa katika nchi.
K. Bwana wa majeshi yu pamoja nasi, Mungu wa Yakobo ni ngome yetu.
Shangilio la Injili
Amo. 5:14Injili
Yn. 5:1-3, 5-16Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (2)
Theopista Mtove · 3 Aprili 2019
Asante kwa kuniunga naomba mnijuze Mtakatifu wa tarehe 2/4/1976
Theopista Mtove · 3 Aprili 2019
Asante kwa kuniunga naomba mnijuze Mtakatifu wa tarehe 2/4/1976