Jumanne ya 7 ya Mwaka
· Mwaka C · Juma la 3 la Zaburi
Somo la Kwanza
Ybs 2:1-11Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zaburi 37:3-4.18-19.27-28.39-40Umtumaini BWANA ukatende mema,
Ukae katika nchi, upendezwe na uaminifu.
Nawe utajifurahisha kwa BWANA,
Naye atakupa haja za moyo wako.
(K)Umkabidhi BWANA njia yako, Pia umtumaini, naye atafanya.
BWANA anazijua siku za wakamilifu,
Na urithi wao utakuwa wa milele.
Hawataaibika wakati wa ubaya,
Na siku za njaa watashiba.
(K)Umkabidhi BWANA njia yako, Pia umtumaini, naye atafanya.
Jiepue na uovu, utende mema,
Na kukaa hata milele.
Kwa kuwa BWANA hupenda haki,
Wala hawaachi watauwa wake.
Wao hulindwa milele,
Bali mzao wa wasio haki ataharibiwa.
(K)Umkabidhi BWANA njia yako, Pia umtumaini, naye atafanya.
Na wokovu wa wenye haki una BWANA;
Yeye ni ngome yao wakati wa taabu.
Naye BWANA huwasaidia na kuwaopoa;
Huwaopoa na wasio haki na kuwaokoa;
Kwa kuwa wamemtumaini Yeye.
(K)Umkabidhi BWANA njia yako, Pia umtumaini, naye atafanya.
Shangilio la Injili
Gal 6:14Mbali na mimi kuwa na utukufu isipokuwa msalabani wa Bwana wetu Yesu Kristo, ambalo dunia imesulubiwa kwangu, na mimi ulimwenguni.
Alleluya.
Injili
Mk 9: 30-37Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni