Jumatano baada ya Epifania
· Mwaka C · Juma la 2 la Zaburi
Somo la Kwanza
1Yon. 4:11-18Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab. 72:1-2,10,12-13Mataifa yote ya ulimwengu, watakusujudia, ee Bwana.
Ee Mungu, mpe mfalme hukumu zako.
Na mwana wa mfalme haki yako.
Atawaamua watu wako kwa haki,
Na watu wako walioonewa kwa hukumu.
K. Mataifa yote ya ulimwengu, watakusujudia, ee Bwana.
Siku zake yeye, mtu mwenye haki atasitawi,
Na wingi wa Amani hata mwezi utakapokoma
Na awe na enzi toka bahari hata bahari,
Toka mto hata miisho ya dunia.
K. Mataifa yote ya ulimwengu, watakusujudia, ee Bwana.
Wafalme wa Tarshisi na visiwa walete kodi,
Wafalme wa Sheba na Seba na watoe vipawa.
Naam, wafalme wote na wamsujudie;
Na mataifa yote wamtumikie.
K. Mataifa yote ya ulimwengu, watakusujudia, ee Bwana.
Kwa maana atamwokoa mhitaji aliapo,
Na mtu aliyeonewa iwapo hana msaidizi
Atamhurumia aliye dhaifu na maskini,
Na nafsi za wahitaji ataziokoa.
K. Mataifa yote ya ulimwengu, watakusujudia, ee Bwana.
Shangilio la Injili
Lk. 4:18-19Bwana amenituma kuwahubiri maskini habari njema, na kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao.
Aleluya.
Injili
Mk. 6:45-52Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni