Siku ya tano ya Oktava ya kuzaliwa Bwana
· Mwaka C · Juma la 1 la Zaburi
Somo la Kwanza
1Yoh. 2:3-11Wapenzi, siwaandikii amri mpya, ila amri ya zamani mliyokuwa nayo tangu mwanzo. Na hiyo amri ya zamani ni neno lile mlilolisikia.
Tena nawaandikia amri mpya, neno lililo kweli ndani yake na yenu; kwa kuwa giza linapita na vile nuru ya kweli imekwisha kung’aa. Yeye asemaye kwamba yumo nuruni, naye amchukia ndugu yake, yumo gizani hata sasa. Yeye ampendaye ndugu yake, akaa katika nuru, wala ndani yake hamna kikwazo. Bali yeye amchukiaye ndugu yake, yu katika giza, tena anakwenda katika giza, wala hajui aendako, kwa sababu giza imempofusha macho.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab. 96:1-3,5-6Mbingu na zifurahi, nchi na ishangilie.
Mwimbieni Bwana wimbo mpya,
Mwimbieni Bwana, nchi yote,
Mwimbieni Bwana, libarikini jina lake.
K. Mbingu na zifurahi, nchi na ishangilie.
Tangazeni wokovu wake siku kwa siku,
Wahubirini mataifa habari za utukufu wake,
Na watu wote habari za maajabu yake.
K. Mbingu na zifurahi, nchi na ishangilie.
Lakini Bwana ndiye aliyezifanya mbingu,
Heshima na adhama ziko mbele yake,
Nguvu na uzuri zimo katika patakatifu pake.
K. Mbingu na zifurahi, nchi na ishangilie.
Shangilio la Injili
ShangilioSiku takatifu imetung’aria: Enyi mataifa, njoni mkamwabudu Bwana: Kwa sababu mwanga mkubwa umeshuka duniani.
Aleluya.
Injili
Lk. 2:22-35Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni