Ijumaa ya 29 ya Mwaka
· Mwaka B · Juma la 1 la Zaburi
Somo la Kwanza
Efe. 4:1 – 6Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab. 24:1 – 6Hiki ndicho kizazi cha wakutafutao, Ee Bwana.
Nchi na vyote viijazavyo ni mali ya Bwana,
Dunia na wote wakaao ndani yake.
Maana ameiweka misingi yake juu ya bahari,
Na juu ya mito ya maji aliithibitisha.
K. Hiki ndicho kizazi cha wakutafutao, Ee Bwana.
Ni nani atakayepanda katika mlima wa Bwana?
Ni nani atakayesimama katika patakatifu pake?
Mtu aliye na mikono safi na moyo mweupe,
Asiyeiinua nafsi yake kwa ubatili,
Wala hakuapa kwa hila.
K. Hiki ndicho kizazi cha wakutafutao, Ee Bwana.
Atapokea Baraka kwa Bwana,
Na haki kwa Mungu wa wokovu wake.
Hiki ndicho kizazi cha wamtafutao,
Wakutafutao uso wako, Ee Mungu wa Yakobo.
K. Hiki ndicho kizazi cha wakutafutao, Ee Bwana.
Shangilio la Injili
Efe. 1:17, 18Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo, awape roho ya hekima mjue tumaini la mwito wake.
Aleluya.
Injili
Lk. 12:54-59Na mbona ninyi wenyewe kwa nafsi zenu hamwamui yaliyo haki? Maana, unapofuatana na mshitaki wako kwenda kwa mwamuzi, hapo njiani fanya bidi kupatanishwa naye, asije akakuburuta mpaka mbele ya kadhi; yule kadhi akakutia mikononi mwake mwenye kulipiza, na yule mwenye kulipiza akakutupa gerezani. Nakuambia, Hutoki humo kamwe hata uishe kulipa senti ya mwisho.
Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni