Jumanne ya 28 ya Mwaka
· Mwaka B · Juma la 4 la Zaburi
Somo la Kwanza
Gal 5:1-6Katika ungwana huo kristo alituandikia huru kwa hiyo simameni wala msinaswe tena chini ya kongwa la utumwa. Tazama mimi Paulo nawambia ninyi ya kwamba mkitahiriwa, Kristo hatawafaidia neno. Tena namshuhudia kila mtu atahiriwaye,kwamba ni wajibu wake kutimiza torati yote.Mmetengwa na kristo mtakao kuhesabiwa haki kwa sheria ; mmeanguka na kutoka katika hali ya neema. Maana sisi kwa roho tunalitazamia tumaini la haki kwa njia ya Imani.Maana katika Kristo Yesu kutahiriwa hakufai neno,wala kutotahiriwa , bali Imani itendayo kazi kwa upendo.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 119:41,43-45,47-48Ee bwana fadhili zako zinifikie na mimi
Ee bwana fadhili zako zinifikie na mimi
Naam wokovu wako sawasawa na ahadi yako
Nami nitamjibu neno anilaumuye
Kwa maana nalitumainia neno lako
K. Ee bwana fadhili zako zinifikie na mimi
Nami nitaitii milele na milele
Naam milele na milele
Nami nitakwenda panapo nafasi
Kwa kuwa nimejifunza mahusia yako
K. Ee bwana fadhili zako zinifikie na mimi
Nami nitajifurahisha sana kwa maagizo yako
Ambayo nimeyapenda
Na mikono yangu nitayainulia
Maagizo yako niliyoyapenda
Nami nitazitafakari amri zako.
K. Ee bwana fadhili zako zinifikie na mimi
Shangilio la Injili
Zab 119:135Umwangazie mtumishi wako uso wako,
Na kunifundisha amri zako.
Aleluya.
Injili
Lk. 11:37-41Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni